Posts

Image
  KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR ATOA NENO KWA AJILI YA MAADHIMISHO YA SIKU 16 . NA MWANDISHI WETU. JESHI  la Polisi Zanzibar limesema linasimama mstari wa mbele kuhakikisha kesi za ukatili wa kijinsia zinashughulikiwa kwa haraka na haki kupatikana kwa wahanga. Ámeyyseama hayo wakati akitoa taarifa za takwimu, za matukio ya ukatili wa kijisia ambayo bado yanaripotiwa kwa kiwango cha kutisha ambavyo hufanyika majumbani, mashuleni, kazini, na katika maeneo ya umma.  Amesema jamii inapaswa kutafakari kwa kina madhara ya ukatili wa kijinsia katika jamii zetu na kuchukua hatua madhubuti za kulinda haki za wanawake na wasichana, ambao ni nguzo muhimu za maendeleo ya taifa letu. Amesema hali hii inahitaji juhudi za pamoja kati ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, asasi za kiraia, viongozi wa dini, na jamii  ili kuelimisha watu u athari za ukatili wa kijinsia na kukuza utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu.  " Ni ukweli usiopingika kuwa ukatili dhidi ya wanawake ...
Image
  TAMWA: WAANDISHI TUMIENI KALAMU ZENU KUSAIDIA KUINUA   VIPAJI VYA MICHEZO VYA WANAWAKE .            WAANDISHI wa habari za michezo kisiwani pemba wametakiwa kuongeza juhudi katika kuandika habari hizo kwa wanawake ili kuwezesha ushiriki sawa wa jinsi zote  kuzifikia fursa . Ameyasema hayo Afisa tathmini na ufuatiliaji kutoka TAMWAZanzibar Mohammed khatib wakati wa kikao cha ufuatiliaji wa utendaji kazi kwa waandishi hao.   “TAMWA inaamini waandishi wa habari wana uwezo mkubwa wakuhamasisha jamii katika harakati tofauti ikiwemo wanawake kwenye kushiriki michezo.” “Mbali ya changamoto zinazowakabili wanawake katika kushiriki michezo ni vyema kwenu waandishi kuchukua changamoto mulizoziona kwenye jamii na kuzipeleka sehemu husika ili kushirikiana kuwasaidia   wanawake kushiriki michezo”aliongeza. Akitaja lengo la tathmini hiyo afisa programu kutoka TAMWAZanzibar Khairat haji ali amesema ni kuangalia maendeleo ya mradi n...
Image
NA KHADIJA ALI YUSSUF, MADRASA EARLY CHILD HOOD: WAHITIMU TUMIENI FURSA YA MAFUNZO  Wahitimu wa mafunzo ya ualimu wa maandalizi kwa ngazi ya cheti kutoka early childhood Pemba wametakiwa kutumia ujuzi wa mafunzo waliyopatiwa ili lengo la wizara ya elimu liweze kufikiwa.  ‎Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Zanzibar Maalim Othman Omar Othman katika mahafali ya wahitimu hao  katika  Ukumbi wa ZSSF Tibirinzi chake chake Pemba. ‎ ‎Amesema ubunifu na  taaluma  waliopatiwa wakati wa masomo yao iwapo wataitumia ipasavyo  wataweza kupata wanafunzi wenye ufaulu mzuri na lengo la wizara litaweza kufikiwa Kwa kuwa na wataalamu Bora katika sekta mbali mbali. ‎ ‎Aidha Mkurugenzi huyo amewaomba wahitimu hao kutotosheka na elimu walioipata hapo na badala yake waendelee kujifunza kupitia ngazi mbali mbali kwani lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuona sekta ya elimu inakua siku Hadi siku kwa kujenga vyuo kuanzia ngazi msingi hadi vyuo vikuu K...
Image
 TAMWA YAENDELEA KUWANOA WAHAMASISHAJI JAMII PEMBA. Wahamasishaji jamii  kisiwani Pemba wametakiwa kutumia fursa za mafunzo waliyopewa  kua mabalozi wazuri ili kuleta mabadiliko na kufikia lengo la uwiano sawa wa 50/50 kwenye ngazi za maamuzi. Ameyasema hayo Afisa kutoka afisi ya msajili  wa taasisi zisiso za kiserikali NGO’s Sada Aboubakar Khamis  wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wahamasishaji jamii kwa niaba ya mrajisi wa taasisi hiyo. Amesema kwa vile demokrasia haikumbaguwa mtu katika kushika nafasi za uongozi ni vyema kuepuka mifumo dume na dhana potofu ya kuwa mwanamke hafai kuwa kiongozi. Alisema wakati umefika kwa wanawake kuwa na msimamo mmoja wa kuhakikisha wanashika nafasi mbalimbali za uongozi ili nao waweze kutowa maoni katika ngazi za maamuzi. “Wanawake tuamke tusikae nyuma tunapotoka ni mbali ila kwa sasa ni muda wa kutumia fursa zilizopo kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi",alisema Awali akitoa tathmini ya ufikiwaji wa awamu ya 2 ...
Image
  KATUMENI YALIA UKOSEFU WA ELIMU YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA. Ukosefu wa elimu ya matumizi ya nishati safi   ya kupikia bado ni changamoto inayopelekea baadhi ya wakaazi wa Katumeni Shehiya ya Makombeni, kuendelea kutumia kuni kama ni nyenzo kuu ya kukidhi mahitaji. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi mwanajamii Mtumwa Abdallah Mohammed na Mohammed Faki Ali, wamesema hawajawahi kufikiwa kupewa elimu hiyo hali inayowapa ugumu kutumia nishati safi ya kupikia katika kuandaa chakula cha siku. “ Matumizi ya nishati safi ya kupikia hasa vijijini inahitaji elimu ya kutosha kwani hatuna uzoefu na utumiaji wake,kufanya hivyo kutatupa urahisi wa kutumia sambamba na kujikinga na madhara yatokanayo na matumizi ya nishati isiyo salama” walisema wanajamii. Mwashumu Makame Haji,Sheha wa Makombeni amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo Shehiyani hapo, amechukua nafasi kuielimisha jamii kwa kusema “Gesi haina madhara kama jamii inavyoeleza, hivyo ni vyema kwa   taa...
Image
    TAMWA:: WAANDISHI TUMIENI KALAMU ZENU  KUHAMASISHA WANAWAKE KUPITIA  ZANADAPT. Waandish i wa habari Kisiwani Pemba wametakiwa kutumia fursa za mrdi wa ZanAdapt kuwahamasishawanawake kushiriki kwenye demokrasia na uongozi. Ameyasema hayo Afisa mawasilino TAMWA Zanzibar Nafda Hindi  wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi hao yanayoangazia mabadiliko ya tabianchi na wanawake. Akiwakilisha mada ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji kwa wanawake Ali Mbarouk   amesema muda umefika kwa waandishi kuandaa mikakati itakayohamasisha wanawake kutumia fursa za mradi kukabiliana na changamoto za tabianchi . Ameongeza kuna juhudi nyingi zinazochukuliwa na wanawke katika kukabiliana na tabianchi ikiwemo upandaji wa mikoko na mikarafuu   hivyo ni vyema kwa waandishi kutumia kalamu zao kupaza sauti za wanawake ili kuongeza ushiriki na ushirikishwaji. Habiba Zarali Rukuni na Is haka Rubea wamesema wanafurahi kuapata mafunzo ya mabadiliko ya ...