TAMWA: WAANDISHI TUMIENI KALAMU ZENU KUSAIDIA KUINUA VIPAJI VYA MICHEZO VYA WANAWAKE.
WAANDISHI wa habari za michezo kisiwani pemba wametakiwa kuongeza juhudi katika kuandika habari hizo kwa wanawake ili kuwezesha ushiriki sawa wa jinsi zote kuzifikia fursa .
Ameyasema
hayo Afisa tathmini na ufuatiliaji kutoka TAMWAZanzibar Mohammed khatib wakati
wa kikao cha ufuatiliaji wa utendaji kazi kwa waandishi hao.
“TAMWA inaamini waandishi wa habari wana uwezo
mkubwa wakuhamasisha jamii katika harakati tofauti ikiwemo wanawake kwenye
kushiriki michezo.”
“Mbali ya
changamoto zinazowakabili wanawake katika kushiriki michezo ni vyema kwenu waandishi
kuchukua changamoto mulizoziona kwenye jamii na kuzipeleka sehemu husika ili
kushirikiana kuwasaidia wanawake kushiriki
michezo”aliongeza.
Akitaja
lengo la tathmini hiyo afisa programu kutoka TAMWAZanzibar Khairat haji ali
amesema ni kuangalia maendeleo ya mradi na kuweka taarifa za matokeo ya mradi huo.
“Awamu iliyopita
hali haikua nzuri ila kwa sasa inaridhisha, hivyo ni muhimu kuendelea ili
kuhakikisha ushiriki wa wanawake kwenye michezo unaongezeka.”
Kwa upande Waandishi
wa habari waliopo kwenye mradi huo wamesema bado changamoto za uhaba wa viwanja
na mtazamo hasi kwa baadhi ya jamii pamoja na ushirikishwaji bado ni vizingiti
kwa watoto wa kike kushiriki michezo.
“Baadhi ya
wazazi wanatamani watoto wao washiriki michezo ila mazingira ya viwanja sio
rafiki ya wao kushiriki michezo.” Alisema habiba zarali.
“Mavazi pia
ni kikwazo kwa wazazi kuwaruhusu watoto wa kike kushiriki michezo.” Alisema
fatma hamad.
Michezo kwa
maendeleo ni mradi unaofadhiliwa na shirika la maendeleo ya kimataifa la
Ujerumani( GIZ) na kutekelezwa na taasisi tatu @TAMWA_Zanzibar , Taasisi ya Wanasheria Wanawake Zanzibar,@ ZAFELA na
Center for Youth Dialogue @CYD,wenye lengo la kukuza usawa wa
kijinsia katika michezo.
Comments
Post a Comment