NA KHADIJA ALI YUSSUF,

MADRASA EARLY CHILD HOOD: WAHITIMU TUMIENI FURSA YA MAFUNZO 


Wahitimu
wa mafunzo ya ualimu wa maandalizi kwa ngazi ya cheti kutoka early childhood Pemba wametakiwa kutumia ujuzi wa mafunzo waliyopatiwa ili lengo la wizara ya elimu liweze kufikiwa. 

‎Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Zanzibar Maalim Othman Omar Othman katika mahafali ya wahitimu hao  katika  Ukumbi wa ZSSF Tibirinzi chake chake Pemba.
‎Amesema ubunifu na  taaluma  waliopatiwa wakati wa masomo yao iwapo wataitumia ipasavyo  wataweza kupata wanafunzi wenye ufaulu mzuri na lengo la wizara litaweza kufikiwa Kwa kuwa na wataalamu Bora katika sekta mbali mbali.
‎Aidha Mkurugenzi huyo amewaomba wahitimu hao kutotosheka na elimu walioipata hapo na badala yake waendelee kujifunza kupitia ngazi mbali mbali kwani lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuona sekta ya elimu inakua siku Hadi siku kwa kujenga vyuo kuanzia ngazi msingi hadi vyuo vikuu Kwa lengo la kukuza elimu.
‎Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Early Childhood Programme Zanzibar Maalim Haji Ali Hamad ameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanapotekeleza miradi yao ya elimu kuzingatia na watu wenye mahitaji maalum ili kupingunguza changamoto zinazowakabili.
‎Akisoma Risala ya wahitimu hao Asmaa Khamis Hamad ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya awamu ya 8 Kwa kutoa fursa nyingi za ajira sambamba na wahitimu hao kuwa walimu bora Kwa maslahi ya Taifa.
‎Pia amewataka walim walio hitimu katika mafunzo hayo kuyafanyia juhudi za kujituma zaid ili mazingira ya Madarasa yaawali yaedeleye kuwa na ubora edelevu  kwa faida ya sasa nasiku zijazo.



‎Jumla ya wahitimu 120 kutoka Skuli 84 za Unguja na Pemba wamepatiwa Mafunzo hayo Kwa ufadhili Mradi wa Foundation of Learnig wa nchini Canada

Comments