KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR ATOA NENO KWA AJILI YA MAADHIMISHO YA SIKU 16 .


NA MWANDISHI WETU.

JESHI la Polisi Zanzibar limesema linasimama mstari wa mbele kuhakikisha kesi za ukatili wa kijinsia zinashughulikiwa kwa haraka na haki kupatikana kwa wahanga.

Ámeyyseama hayo wakati akitoa taarifa za takwimu, za matukio ya ukatili wa kijisia ambayo bado yanaripotiwa kwa kiwango cha kutisha ambavyo hufanyika majumbani, mashuleni, kazini, na katika maeneo ya umma. 

Amesema jamii inapaswa kutafakari kwa kina madhara ya ukatili wa kijinsia katika jamii zetu na kuchukua hatua madhubuti za kulinda haki za wanawake na wasichana, ambao ni nguzo muhimu za maendeleo ya taifa letu.

Amesema hali hii inahitaji juhudi za pamoja kati ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, asasi za kiraia, viongozi wa dini, na jamii  ili kuelimisha watu u athari za ukatili wa kijinsia na kukuza utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu.

 " Ni ukweli usiopingika kuwa ukatili dhidi ya wanawake na wasichana sio tu ukiukwaji wa haki za binadamu, bali pia ni kikwazo kikubwa katika kufikia maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi". Alisema

Aidha ametoa wito kwa viongozi wa serikali, viongozi wa dini, wazazi, walimu, na vijana kuwa mabalozi wa kupinga ukatili wa kijinsia. kuhakikisha wanawake na wasichana wanaishi kwa amani, usalama, na heshima, wakitimiza ndoto zao bila hofu ya kunyanyaswa au kudhulumiwa.

Comments