TAMWA:: WAANDISHI TUMIENI KALAMU ZENU  KUHAMASISHA WANAWAKE KUPITIA 

ZANADAPT.


Waandishi wa habari Kisiwani Pemba wametakiwa kutumia fursa za mrdi wa ZanAdapt kuwahamasishawanawake kushiriki kwenye demokrasia na uongozi.

Ameyasema hayo Afisa mawasilino TAMWA Zanzibar Nafda Hindi  wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi hao yanayoangazia mabadiliko ya tabianchi na wanawake.

Akiwakilisha mada ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji kwa wanawake Ali Mbarouk  amesema muda umefika kwa waandishi kuandaa mikakati itakayohamasisha wanawake kutumia fursa za mradi kukabiliana na changamoto za tabianchi .

Ameongeza kuna juhudi nyingi zinazochukuliwa na wanawke katika kukabiliana na tabianchi ikiwemo upandaji wa mikoko na mikarafuu  hivyo ni vyema kwa waandishi kutumia kalamu zao kupaza sauti za wanawake ili kuongeza ushiriki na ushirikishwaji.

Habiba Zarali Rukuni na Is haka Rubea wamesema wanafurahi kuapata mafunzo ya mabadiliko ya tabianchi na wanawake kwani yatawaongezea ufanisi katika utekelezaji wa kazi zao.

.Jumla ya waandishi 12 wameshiriki kwenye mafunzo hayo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wa kuandika habari za tabianchi na wanawake yamefanyika Pemba katika ofisi za @TAMWA _Zanzibar. 










Comments