KATUMENI YALIA UKOSEFU WA ELIMU YA MATUMIZI YA
NISHATI SAFI YA KUPIKIA.
Ukosefu wa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia bado ni changamoto inayopelekea baadhi ya wakaazi wa Katumeni Shehiya ya Makombeni, kuendelea kutumia kuni kama ni nyenzo kuu ya kukidhi mahitaji.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi mwanajamii
Mtumwa Abdallah Mohammed na Mohammed Faki Ali, wamesema hawajawahi kufikiwa
kupewa elimu hiyo hali inayowapa ugumu kutumia nishati safi ya kupikia katika
kuandaa chakula cha siku.
“Matumizi ya nishati
safi ya kupikia hasa vijijini inahitaji elimu ya kutosha kwani hatuna uzoefu na
utumiaji wake,kufanya hivyo kutatupa urahisi wa kutumia sambamba na kujikinga
na madhara yatokanayo na matumizi ya nishati isiyo salama” walisema wanajamii.
Mwashumu Makame Haji,Sheha wa Makombeni amekiri
kuwepo kwa changamoto hiyo Shehiyani hapo, amechukua nafasi kuielimisha jamii
kwa kusema
“Gesi
haina madhara kama jamii inavyoeleza, hivyo ni vyema kwa taasisi husika kupunguza gharama ili wanajamii
wa vijijini waweze kutumia”. Alisema sheha wa Makombeni.
Moh’d Faki Saleh ,daktari kutoka Hospiali ya
Abdallah Mzee Mkoani, amekiri kuwepo athari lukuki zinazosababishwa na utumiaji
wa kuni na kuongeza….
“Ni
vyema kila mmoja kusimama kwa nafasi yake kuhakikisha wanawake wananusurika
kiafya kutokana na matumizi ya kuni”.aliongeza dkt Mohammed.
Aisha Abdalla Rashid afisa bayoanway idara ya
mazingira pemba amekiri uwepo wa wananchi wengi kutokua na elimu hiyo na
kuamini kua nishati safi ya kupikia ni gesi tu.
“Mbali
ya nishati ya gesi umeme , Bayo gas na makaa ya takataka nazo ni salama kwa
kupikia , hivyo ndani ya miezi sita ijayo wananchi wote wa Mkoani wataweza
kufikiwa ili kupatiwa elimu hiyo”.Alisema
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia
Suluhu Hassan akizindua Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia
mwaka huu, Amesema nguvu kubwa ya taifa inaathirika kiafya kwa matumizi ya kuni na Makaa.
Kwani, watanzania zaidi
ya 33,000 hupoteza maisha kila mwaka kwa tatizo la mfumo wa kupumua ambao
huchangiwa na matumizi ya kuni za kupikia wanawake wakiongoza kwenye idadi
hiyo.
Shehiya ya Makombeni,ina zaidi ya wakaazi 2100 ambapo
takriban asilimia 90 wanatumia kuni kwa kupikia.
Comments
Post a Comment